
Mwenyekiti wa Kamati namba tisa (9) ya Bunge Maalum la Katiba, Kidawa Hamid Salehe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Bunge mjini Dodoma kuhusu mambo yaliyojiri katika Kamati yake wakati wa kuchambua sura ya kwanza na ya sita kwenye rasimu ya Katiba. Kulia ni Makamu wake, William Ngeleja. Kamati hiyo imepitisha ibara zote za sura hizo kwa kura za 2/3.