Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Assah Mwambene)(kulia) na Ofisa Habari wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM), Hassan Abbas (kushoto) wakitoa ufafanuzi kwa watoto waliofika kwenye banda la wizara hiyo kuhoji masuala mbalimbali ikiwemo kuhusu upatikanaji wa viza, namna ya kusafiri nje ya nchi na haki za watanzania walioko nje ya nchi. APRM na taasisi nyingine za wizara hiyo; Chuo cha Diplomasia na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) vinashiriki kwa pamoja katika maonesho hayo ya miaka 50 ya Uhuru yanayofanyika Dar es Salaam.