Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge, ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma.
Mbunge wa Bumbuli January Makamba akiwasilisha Hoja binafsi kuhusu sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi aliyoitoa chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge toleo la 2007 ya kuliomba bunge kuazimia kwa kauli moja, kuitaka Serikali katika mkutano ujao wa saba kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini kutokana na adha wanazopata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi kwenye nyumba hizo. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwasalimia viongozi na wachezaji wa timu ya Villa Squard ya Kinondoni jijini Dar es Salaam waliofika bungeni hapo kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na bunge. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Hijra ya mjini Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.