MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu wa nafasi ya urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Licha ya ushindani huo kuwa mkali hadi sasa Rais Barack Obama anaongoza kwa ushindi wa majimbo 172 huku mpinzani wake Mitt Romney akiwa amejikusanyia majimbo 163.
Rais Obama wa chama cha anaongoza ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008. Taarifa zinazohusiana Mitt Romney wa Republican yeye ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Hata hivyo mshindi wa jumla wa uchaguzi huo huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakiendelea kutolewa.
Pamoja na matokeo hayo ya awali kura za maoni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo zilionesha kinyang’anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema. Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita. Mshindi wa uchaguzi huo anatakiwa kupata kura 270 katika majimbo yote.