Matokeo ya Awali Uchaguzi wa Ubunge Arusha Mjini na Handeni Mjini
Taarifa za awali ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha Mjini; idadi ya wapiga kura walioandikishwa 317,814, Waliopiga kura 105,800 ikiwa sawa na 32.83%, Kura halali 104,353, Kura zilizoharibika 1447.
MATOKEO;
NAVOI MOLLEL ACT kura 342 sawa na 0.3%.
PHILEMON OLAIS MOLLEL CCM kura 35,907 sawa na 34.4%.
GODBLESS JONATHAN LEMA CDM kura 68,848 sawa na 65.9%.
ZUBERI MWINYI HAMIS CUF kura106 sawa na 0.1%.
MKAMA RASHID JARALIA kura 43 sawa na 0.04%.
Matokeo Jimbo la Handeni mjini; Waliojiandikisha kata zote 12 ni 38,597, waliopiga kura 16,046.
Matokeo; Kigoda Omar Abdullah wa CCM amepata kura 10,315 (75.90%)
Shundi Remmy Aidan wa CUF amepata kura 2,419 (17.80%),
Daudi Killo Lusewa wa CHADEMA amepata kura 648 (4.77%)
Hassan Mohamedi wa ADC amepata kura 184 (1.35%)
Na Bakari Makame Semndil wa TLP amepata kura 19 (0.14%).