Matokeo mbalimbali ya Uchaguzi Serikali za Mitaa

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila sababu za msingi

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila sababu za msingi

MWANGA Mtaa wa Lwami CHADEMA 55, CCM 35, Mererani CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati ya 8 na Kitongoji cha Endulele CHADEMA 170, CCM 130. Jijini Dar es Salaam eneo la Tabata Kimanga Chadema imeshinda kwa Mwenyekiti na wajumbe wake wote huku matokeo ya awali vijiji na vitongoji Wilaya ya Iringa vijijini ya Desemba 14, 2014 yakionesha:-

-Kata zilizopo wilayani ni 28. *Vijiji vilivyopo wilayani ni 133, CCM imeshinda vijiji 89,
CHADEMA imeshinda vijiji 02. *Vitongoji vilivyopo wilayani ni 747, CCM imeshinda vitongoji 698 na CHADEMA imeshinda vitongoji 15 tu. *Matokeo hayo ni ya Kata 24, bado kujumlisha matokeo ya Kata nne.

Matokeo kamili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. CCM – 77, Chadema – 72, NCCR – 2.
Lakini Mitaa 77 + 28 (CCM tulipita bila kupingwa) = 105. Mitaa 2 uchaguzi utafanyika wiki ijayo.
Mitaa hiyo ipo Mwansekwa na Itiji.

Jiji la Mbeya lina jumla ya Mitaa 181. Monduli; Kitongoji Kambi ya Mkaa CHADEMA 27
CCM 13. Mwanga Mtaa wa Lwami; CHADEMA 55, CCM 35, Ushirombo mjini; CHADEMA inaongoza vitongoji 10
CCM inaongoza vitongoji 4, Moshi Manispaa; Kitongoji Longuo A CHADEMA 206 CCM 66

Mbozi Mtaa wa Mbugani, CHADEMA 227, CCM 160

Mbozi; Mtaa Masaki, CHADEMA 99, CCM 44

Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole, CHADEMA 240, CCM 198

Ukonga- Mtaa wa Kivule Majohe CHADEMA 231, CCM 77

Musoma Vijijini- Kijiji cha Muhoji, CHADEMA 197 na CCM 464

Ubungo- Mtaa wa Msewe, CHADEMA 683, CCM 356

Kinondoni- Mwenge Nzasa, CHADEMA 344 na CCM 318

Tarime Forodhani boda (kitongoji)
CHADEMA 289
CCM 90

Tarime Forodhani Kijiji
CHADEMA 312
CCM 99

Monduli Mto wa Mbu Kijiji Jangwani
CHADEMA 147
CCM 124

Mwanga Kitongoji Mgagao
CHADEMA 56
CCM 32

Rorya- Mtaa Ngasaro
CHADEMA 480
CCM 360

Arumeru Mash. Mtaa wa Manyata
CHADEMA 168
CCM 91

Mbinga Ruvuma, Kijiji cha Mkinga, CCM 313, CUF 41, Karatu bomani CCM 177 Chadema 251, Karatu kati CCM 109 Chadema 281 na TFA CCM 199 Chadema 358

Wakazi wa Mtaa wa Migombani, Uliopo Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka gari la Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza kusitisha uchaguzi wa serikali ya mitaa kimya kimya.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa kawekwa mtukati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila sababu ya msingi. waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo cha kupigia kura cha Migombani.
 Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea
 Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi wa Migomabni akielezea sababu za kusimamisha uchaguzi huo kwa muda kutokana na kusubilia barua ya kumtaka kuendelea na uchaguzi kutoka kwa afisa mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka kujaribu kusitisha Uchaguzi huo kwa kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.
Hii ndio barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea inavyosomeka ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi wa migombani kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa uchaguzi unaendelea
Wakazi wa Mtaa wa migombani, Kata ya Segerea wakimzuia Afisa mtendaji huyo kuondoka mpaka atangaze tena kuwa uchaguzi unaendelea.Picha na Josephat  Lukaza wa Lukaza Blog


Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.

Hali ya Kushtusha imetokea katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani Mara baada ya Afisa Mtendaji huyo kuja na kutangaza kimyakimya Kuwa UChaguzi huo umesitishwa, Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kusikia ndipo walipoanza sasa kutafuta mchawi na kumtia nguvuni afisa mtendaji huyo wa mtaa kwa kutaka kujua sababu za msingi zinazopelekea yeye kuja kutangaza kusitisha uchaguzi huo.

Afisa mtendaji huyo baada ya kuulizwa sababu za msingi alijitetea kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya ilala. Mara baada ya Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna dalili za kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo walipomuweka mtu kati na kumtaka Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa maandishi kuwa uchaguzi unaendelea ndipo wakazi hao walipomuweka mtu kati na kuhakikisha anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.

Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kwenda nae katika ofisi ya kata kwaajili ya kugonga muhuri kuthibitisha Uchaguzi huo kuendelea ndipo uchaguzi ukaendelea na muda huu zoezi la kuhesabu kura linaendelea