BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Kidato cha Sita, 2016 huku shule 10 zilizofanya vizuri ni pamoja na Sekondari za Kisimiri-Arusha, Feza Boys-Dar es Salaam, Alliance Girls-Mwanza, Feza Girls-Dar es Salaam, Marian Boys-Pwani, Tabora Boys -Tabora, Kibaha -Pwani, Mzumbe-Morogoro, Sekondari ya Ilboru-Arusha na Sekondari ya Tandahimba ya Mkoani Mtwara.
Kwa mujibu wa matokeo hayo Shule kongwe za Serikali ambazo zilikuwa zimesahaulika zimeonekana kuamka na kuanza kufanya vizuri zikiwemo Sekondari za Tabora Boys ya Tabora, Sekondari ya Kibaha ya Pwani, Sekondari ya Mzumbe ya Morogoro na Sekondari ya Ilboru ya mkoani Arusha ambazo zote zimeingia katika orodha ya shule 10 zilizoongoza kwa ufaulu kitaifa katika matokeo hayo.
Taarifa hizo zinaonesha shule 10 zilizofanya vibaya: ni Sekondari za Mpendae-Unguja, Ben Bella-Unguja, Tumekuja-Unguja, Green Bird Boys-Kilimanjaro, Jang’ombe-Unguja, Kiembe Samaki-Unguja, Tanzania Adventist-Arusha, Al- Ishan Girls-Unguja, Azania-Dar es Salaam pamoja na Sekondari ya Lumumba-Unguja.
Kwa matokeo zaidi fuata link hii:- NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
au fuata link:- http://tanzania.go.tz/result_acsee_2016/ACSEE2016/index.htm