Matokeo kidato cha nne yatangazwa, 3,303 wafutiwa matokeo

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA), Dk. Jocye Ndalichako

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka 2011/2012, ambapo pamoja na mambo mengine kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 2.6.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Jocye Ndalichako alisema licha ya kupanda kwa kiwango cha ufaulu, tatizo la udanganyifu kwa wanafunzi limeongezeka na julma ya wanafunzi 3,303 wamefutiwa matokeo.

Dk. Ndalichako alisema NECTA imefikia hatua ya kuwafutia matokeo watahiniwa hao baada ya kukutwa na majibu katika nguo na wengine kuandika matusi katika vitabu vyao vya kujibia maswali.

Amesema Baraza la Mitihani linaangalia uwezekano wa kuwachukulia hatua wanafunzi wanaoandika lugha za matusi katika vitabu vya majibu ambapo baraza litawasiliana na mwanasheria mkuu wa Serikali kuona ni hatua gani zitakazo chukuliwa.

Aidha baraza la mitihani Tanzania limetoa onyo kali kwa wamiliki wote wa vituo na shule ambazo zimejihusisha na udanganyifu pamoja na wasimamizi waliobainika katika kuwaandikia watahiniwa. Amesema orodha ya wahusika itapelekwa kwa waajiri wao ili wachukuliwe hatua stahiki. Pata matokeo zaidi kwa kubofya link hapo chini; http://196.44.162.14/necta2011/olevel.htm
http://www.necta.go.tz/results.html