Matnez Apewa Kazi ya Kumnoa Mshambuliaji Eden Hazard

roberto-martinez_2874311b

Meneja wa zamani wa Everton, Wigan na Swansea Roberto Martinez ameteuliwa kuwa meneja mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Martinez, 43, ambaye ni raia wa Uhispania, alifukuzwa Everton mwezi wa tano mwa huu baada ya kufanya kazi Goodison Park kwa miaka mitatu.

Marc Wilmots alijiuzulu wadhifa wake kama meneja wa Ubelgiji mwezi uliopita, wiki mbili baada ya kushindwa na Wales robofainali michuano ya Euro 2016.