RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amemteuwa Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, imeeleza uteuzi wa Chikawe umeanza rasmi tangu Aprili 13, 2016.
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Balozi Chikawe aliteuliwa nafasi ya ubalozi Februari 15, 2016 pamoja na mabalozi wengine watatu ambao hadi sasa bado hawajapangiwa vituo vya kazi. Kiuzoefu Chikawe aliwahi kuwa Mbunge wa Nachingwea 2005 hadi 2015, amewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini.