Matarajio Soko la Mali Zisizohamishika kwa Mwaka 2015

Timu ya Lamudi Tanzania.

Timu ya Lamudi Tanzania.

Matarajio Soko la Mali Zisizohamishika Mwaka 2015

Nini kinatarajiwa kujitokeza katika soko la mali isiyohamishika katika mwaka mpya

MWAKA 2015 inatarajiwa kupungua kwa vikwazo vya kumiliki ardhi nje ya nchi, pia kutakuwa na ongezeko la riba kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa pia biashara ya nyumba na makazi kuhamia kidigitali hasa kupitia simu.

Godlove Nyagawa, Country manager wa Lamudi Tanzania, alifafanua kua kadri mwaka 2014 Kampuni ya Lamudi imekuwa ikitazamia kukua kwa soko la mali hasa katika masoko yanayokua kiuchumi, lakini ndani ya mwaka huu kunamatarajio makubwa zaidi ambayo ni.

1. Mabadiliko ya sheria katika umiliki wa ardhi hasa nchi za kigeni

Katika masoko yanayoibukia kiuchumi, wageni hawana ruhusa ya kumiliki au kununua mali. mfano katika nchi ya Ufilipino, haikuwa na sheria ya kummilikisha ardhi mgeni, lakini katika mwaka 2015 mabadiliko ya kikatiba yanaweza kutokea.

2. Maslahi ya wawekeaji kuongezeka

Godlove alifafanua kwamba, hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wawekezaji wa kigeni na riport kutoka FDI (Foreign Direct Investment) imefafanua kuwa kwa mwaka 2015 wawekezaji wanatarajiwa kuongezeka na kuleta mabadiliko mengi Africa, hiyo pia ni ishara nzuri kwa mwaka huu kuwa na majengo mengi yene ubora wa kisasa, kama inavyoonekana kwa maeneo mengi hapa Tanzania yameshakuwa miji kila siku zinavyongeeka.

3. Tabaka la watu wa kati litaongeza mahitaji na kukua kwa uchumi.
Aliongezea kuwa, Tanzania ni kati ya nchi zilio na watu wa tabaka la kati wengi zaidi kuliko wenye kipato cha juu kwa mwaka 2015 inatarajiwa tabaka hili litakuwa kiuchumi na litasababisha ongezeko la mahitaji ya nyumba, kama inavyojitokeza katika mji wa Indonesia ambapo wao inatarajiwa tabaka hili la kati linaweza kufikia watu Milioni 140 mpaka 2020. Hivyo watu hawa wakiongeza wataleta mabadiliko katika soko hili kwa kasi zaidi.

4. Matumizi ya internet katika simu za mkononi yataleta mageuzi katika soko la mali.
Katika nchi zinazoendelea kiuchumi, watu wanazidi kuongezeka hasa kwa matumizi ya online kadri miaka inavyozidi kwenda, lakini mapinduzi haya ya internet ni tofauti na kipindi cha digitali ilipoingia. Smartphone na tablets zinatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika soko hili ambapo Tanzania inawea kukua kwa kasi zaidi 2015. Katika tovuti ya Lamudi mjini mexico iligundua kuwa zaidi ya watu million 1.1 kufungua tovuti hiyo kupitia simu zao za mkoni.

5. Ukuaji wa kasi wa soko la mali zisizohamishika.

Godlove aliongezea kuwa, Katika tafiti zilizofanywa online katika tovuti ya Lamudi, zimeonyesha kuwa sekta hii itakua kwa kasi hasa kwa mwaka huu, zaidi ya asilimia 23 ya mawakala wa soko hili wanaamini kutakuwa na ukuaji wa soko hilo kwa asilimia 10.

Kwa nchi ya Sri Lanka inatarajiwa kukua kwa asilimia 8 ndani ya mwaka huu, na kupitia mahojiano katika kila nchi inaonyesha kuwa sekta hii itakua kwa kasi ndani ya mwaka huu, kwa nchi ya Tanzania imeonyesha kuwa watu wameaanza kuwa na uelewa wa biashara hii kupitia online na watu wameona umuhimu wa kurahisisha soko hili kupitia kampuni ya Lamudi, hivyo italeta mapinduzi makubwa katika uchumi wa nchi.

KUHUSULAMUDI
Ilizinduliwa 2013, Lamudi ni ya kimataifa inayolenga masoko ya juu ya mali zisizohamishika yanayoibukia kwa haraka- Lamudi inaongezeka kwa sasa inapatikana katika nchi 28 katika Asia, Mashariki ya Kati, Afrika na Amerika ya Kusini, na pia ina idadi ya mali zisizohamishika takribani 600,000 kupitia mtandao wake wa kimataifa. Lamudi ni moja kati ya kampuni zinazoongoza na bora, kutokana na kutoa huduma kwa wauzaji, wanunuzi, wamiliki wa ardhi na wakulima ambapo tovuti hii imekuwa ni salama na rahisi kutumia kupata makazi kupitia online.