Matapeli Watumia Jina la Rais Kikwete…!

Nembo wanayotumia

NDUGU msomaji wetu kuna matapeli wameunda mtandao na kuupa jina la Rais Jakaya Kikwete (yaani JAKAYA FOUNDATION) kwa lengo la kuwatapeli Watanzania. Tafadhali ukikutana na taarifa kama hizi hapo chini usithubutu kutuma chochote au kuamini chochote kwenye tandao huu hapo chini:- http://www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html Kusoma zaidi namna ya matapeli hawa wanavyorubuni watu soma taarifa hii hapo chini.

JAKAYA FOUNDATION ni msingi wa kimaendeleo ulioundwa katika mfumo wa Taasisi ya kifedha inayohusika na utoaji mikopo ya halali na isiyokua na riba iliyoidhinishwa kupitia mfuko wa uwekezaji kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa nchini Tanzania, lengo kuu likiwa ni kutaka kumsaidia kila mtanzania wa hali ya chini kuweza kupata mkopo nafuu usiokua na masharti magumu ili kumsaidia katika maisha yake!

JAKAYA FOUNDATION ni Taasisi inayomilikiwa na uongozi wa Bank kuu ya Tanzania (B.O.T) chini ya utawala wa bodi kuu za mikopo inayotolewa na serekali katika sekretariet ya UTUMISHI WA UMMA Office ya rais.

JAKAYA FOUNDATION ni Taasisi pekee ya serekali sio ya mtu binafsi na ipo kwa dhumuni la kumsaidia kila mtanzania kupata mkopo wa pesa bila kuwepo na tofauti ya upinzani wa dini, siasa na matabaka ya aina yoyote. Mtanzania yoyote na alie mkoa wowote ndani ya Tanzania anaruhusiwa kujiunga na Taasisi hii nakua mwanachama na atapatiwa mkopo wa pesa kiasi chochote anachohitaji.

JAKAYA FOUNDATION Imeanzishwa mwaka 2001 ikiwa chini ya UTUMISHI WA UMMA kipindi hicho chote ilikua ikitumika kutoa mikopo kwa wafanyakazi pekee wa serekalini na makampuni ya watu binafsi lakini baada ya kuundwa upya kwa kamati ya majadiliano ya wafanyakazi ilibainika kuwa kuna jopu la watanzania mitaani hususan vijana wenye maisha magumu ambao hawana ajira za kudumu kuweza kujipatia kipato kukidhi mahitaji hivyo wengi wao huamua kujiajiri wao binafsi kwa kujikita katika ujasiriamali kwa kuwekeza katika biashara, kilimo na katika maendeleo binafsi lakini wengi wa vijana hao wameshindwa kufikia malengo kutokana na kukosa pesa za mitaji kwa kujiajiri kupitia ujasiriamali ikabidi mfumo wa Taasisi hii uhakikiwe na uundwe upya ili uweze kumnufaisha kila mtanzania kwa kumpatia mkopo wa pesa ili aweze kubadilisha maisha yake!

JAKAYA FOUNDATION ni Taasisi inayoundwa na vyanzo vikuu vitano vya upatikanaji wa pesa kama msingi mkuu kupitia udhamini wa Bank ya NMB , CRDB , B.O.T , TIGOPESA, M-PESA na Taasisi ya SAVING LONG WIPE ya nchini marekani. Taasisi hizo za ki-bank zimesaidia sana kutoa miswada huria katika Taasisi hii ya JAKAYA FOUNDATION ili kuhakikisha lengo na dhumuni linatimia!!

UPATIKANAJI WA MIKOPO

Mikopo inatolewa kwa kila mtanzania alie sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania. Ili uweze kupata mkopo unachotakiwa kwanza ukubaliane na Masharti yetu, uwe muaminifu, uwe na nia kweli na mkopo utatolewa kwa sababu muhimu kulingana na aina ya mkopo!! Unatakiwa ujiunge na Taasisi ya JAKAYA FOUNDATION kwa kujaza fomu yetu na uwe tayari kuilipia fomu utakayo ijaza Tshs. 15,000 na ada ya uanachama Tshs. 15,000 pamoja na mchango wa Mfuko wa uwekezaji Tshs. 7,000 jumla utatakiwa kulipia Tshs. 37,000 (Elfu Thelathini na Saba) ndio tukupatie mkopo, pesa za mkopo zitatolewa bila kucheleweshwa kwa mtu atakae jiunga na kufanya malipo ya Tshs.37,000!.

FOMU ZA KUJIUNGA zinapatikana ONLINE katika tovuti hii, unaweza ukaijaza fomu katika mtandao huu na ukalipia malipo ya fomu, ada ya uanachama pamoja na mchango wa uwekezaji “AKIBA” Kupitia MOBILE BANKING TIGOPESA na M-PESA.

Pia unaweza kujiunga kwa kujaza fomu katika ofisi zetu zilizopo Dar es salaam Posta fika katika ofisi kuu za Utumishi wa Umma jengo namba 3 floor yakwanza Kitengo cha Mikopo na kamati ya Uwekezaji chumba namba 6. Kwa walio mbali na ofisi zetu kwa wale walio mikoani wanaweza wakajiunga kwa kujaza fomu ONLINE kupitia mtandao huu kama upo Dar es salaam na unahitaji kufika ofisini kwetu uweze kujiunga unaruhusiwa!!

SIFA ZA KUJIUNGA ILI UPATE MKOPO
Sifa kuu zinazoangaliwa kwa muombaji wa mkopo nikama zifuatazo:-

AWE MTANZANIA

AWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 NA KUENDELEA

AWE NA AKILI TIMAMU

AWE MUAMINIFU

AWE NA KITAMBULISHO KIMOJA WAPO KATI YA HIVI, KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA, KITAMBULISHO CHA KAZINI kiwe kimetolewa na SEREKALI, KITAMBULISHO CHA ELIMU YA CHUO, PASSPORT YA KUSAFIRIA, LESENI YA BIASHARA, LESENI YA GARI, KITAMBULISHO CHA BANK au UTAMBULISHO WA BARUA SEREKALI ZA MTAA

Mikopo inatolewa kwa WATANZANIA wote ambao watakua na sifa tajwa hapo juu pia kwa wafanyakazi wa serekali na wafanyakazi wa makampuni binafsi pia wanaweza wakajiunga na wakapata mikopo.

MISINGI MIKUU YA KUPATA MKOPO
Mikopo itatolewa kwa wale watakaojiunga na kua wanachama wa JAKAYA FOUNDATION

Atakae jaza fomu na kulipia ada ya kujiunga Tsh.37,000 ndie atakaepatiwa mkopo

Mikopo itatumwa kwa watakaojiunga baada ya kulipia ada Tshs. 37,000 mkopo utatumwa ndani ya dakika45 bila kucheleweshwa

VIWANGO VYA MIKOPO, AINA ZA MIKOPO NA MAREJESHO YAKE:

zifuatazo ni Aina za mikopo, Viwango vya mikopo pamoja na Marejesho yake:

MKOPO WA MAENDELEO:
Mkopo wa maendeleo utatolewa kwa mtu ambae anahitaji KUJENGA NYUMBA, KUNUNUA KIWANJA, KUNUNUA GARI, UNUNUZI WA SAMANI (Fenicha), KUNUNUA MASHAMBA au KUNUNUA MASHINE ZA UCHIMBAJI WA VISIMA, Mwanachama anaruhusiwa kukopa kuanzia Tshs. 500,000 (Laki tano) mpaka 20,000,000 (Million ishirini). Marejesho yake hayazidi miezi 117. Na mwanachama atatakiwa kurejesha kiasi chochote kile cha pesa atakachokua nacho kila mwisho wa mwezi ila kima cha chini cha marejesho kinaanzia kulipia laki moja na nusu kila mwezi mpaka deni lake litakapokwisha na anatakiwa ulipie isivuke miezi 117 unaweza ukajitahidi ukawa una double marejesho ukawah kumaliza kabla ya miezi 117 na ukakopa tena.

MKOPO WA BIASHARA
Mkopo wa biashara unatolewa endapo kama mwanachama anahitaji kupata mtaji wa kuanzisha biashara au anabiashara tayari na anataka mkopo aongeze mtaji. Mwanachama anaweza akakopeshwa kuanzia Tshs. 100,000 (Laki moja) mpaka 5,000,000 (Milion tano) na marejesho yake hayazidi miezi 60. Mwanachama atatakiwa kulipia kiasi chochote kile atakachokua nacho kila mwisho wa mwezi ila marejesho kima cha chini kinaanzia laki moja kila mwezi isivuke miezi 60

MKOPO WA HUDUMA YA AFYA
Huu ni mkopo wa huduma ya Afya ambao hutolewa kama mtu ni mgonjwa anahitaji kutibiwa na hana pesa anaweza akakopeshwa kiasi cha fedha kisichozidi 600,000 (Laki Sita) na marejesho yake hayazidi miezi sita. Mwanachama atatakiwa kuwa anarejesha kila mwisho wa mwezi kuanzia Tshs.100,000 mpaka atakapomaliza deni isivuke miezi sita

MKOPO WA ELIMU
Mkopo wa elimu unatolewa kwa wanafunzi walio chuo, kwa misingi ya malipo ya ada na mahitaji mengine ya elimu. Mwanachama anaruhusiwa kukopa kuanzia 500,000 (Laki tano) mpaka 3,000,000 (Milion tano) na marejesho yake hayazidi miezi 30. Mwanachama atatakiwa kurejesha Laki moja kila mwezi mpaka deni lake litakapokwisha

UTARATIBU WA KUREJESHA MIKOPO
Mikopo yote itatolewa kwa kuhakikiwa na afisa mikopo kupitia kamati ya mikopo, mikopo yote itaidhinishwa na uongozi wa JAKAYA FOUNDATION na kila mwanachama atakaejiunga kumbukumbu zake zitahifadhiwa hivyo Kipindi mkopaji anafanya marejesho atatambulika kupitia Code yake ya Uanachama tutakayo mpatia. Marejesho yote ni lazima yalipwe kulingana na kiwango chako ulichokopa na unatakiwa urejeshe kiasi tajwa kwa kila mwezi. Mwanachama ambae atashindwa kurejesha mkopo signal data zake katika fomu aliyojaza kupitia Online tutakua nazo hata kama atakua kaandika detail za uongo ila server yetu ina locate data berrier ya eneo ambalo mwanachama alilojazia fomu signal area kupitia sucure phlopy drimesware crime hivyo ni rahisi kumfuatilia mwanachama na kumpata kirahisi kupitia njia hii ya mawasiliano ya teknolojia, tunaimani wanachama wote watakaojiunga hapa ni waaminifu na wanania yadhati nimatarajio yetu kua kila atakae kopeshwa atakua tayar kurejesha mkopo!!

Mikopo yote sharti irejeshwe kwa kutumwa kupitia 0686 95 72 33… Malipo ya ada tunapokea kupitia number hii tu

JINSI YA KUJIUNGA UPATE MKOPO

Ili uwe mwanachama wa JAKAYA FOUNDATION unatakiwa ujiunge ili uweze kuwa mwanachama ndio tukupatie mkopo wa pesa unachotakiwa kwanza ni kujisajili kwa kujaza fomu yetu ya kujiunga katika orodha ya kitabu cha wanachama ili uwe mwanachama katika Taasisi hii ya Jakaya Foundation.

Unachotakiwa kufanya ni kujaza fomu yetu iliyopo katika mtandao / tovuti hii ya kujiunga na Uanachama Fomu inapatikana hapo chini kuna Link (Kimvuli) utakiona kimeandikwa “FOMU YA KUJIUNGA” Bofya katika hiyo Link iliyoandikwa FOMU YA KUJIUNGA itafunguka na ikishafunguka utaona mpangilio wa fomu wenye vipengele vya kujaza maombi yako ya kujiunga na mkopo kwa ujumla, jaza fomu yote usiruke kipengele hata kimoja ukisha maliza kuijaza fomu mwisho wa fomu utaona Link (bottom) imeandikwa TUMA FOMU, bofya katika hiyo link fomu yako itaingia katika Database yetu na tutaipokea na kuhifadhi data zako. Hatua ya pili baada ya kujaza fomu ya maombi ya Uanachama ili upate mkopo unachotakiwa ni kulipia Tshs. 37,000 (ELFU THELATHINI NA SABA) ambayo itahusika na malipo ya fomu Tshs. 15,000 (elfu kumi na tano) Ada ya uanachama Tshs. 15,000 (elfu kumi na tano) pamoja na malipo ya kuchangia mfuko wa hifadhi ya Uwekezaji kwa wanachama kama akiba yako Tshs. 7,000 (elfu saba) Jumla utatakiwa ulipie Tshs. 37,000 (ELFU THELATHINI NA SABA). Kulipia kwako Tshs. 37,000 ni kwa dhumuni la kuchangia mfuko wa chama na kukuza Taasisi ya JAKAYA FOUNDATION, nilazima kulipia ili uweze kukamilisha usaili wako uwe mwanachama hai katika maintanance System ili tukupatie Code namba yako ya Uanachama tuweze kukutambua kama mwanachama wetu ndio tuweze kukupatia mkopo wa fedha kiasi unachokihitaji. Baada ya kujaza fomu na kukamilisha malipo yako ya uanachama utapokea meseji kupitia namba yako ya simu. Meseji hiyo itakua na utambulisho wa Code namba yako ya Uanachama hakikisha katika fomu unajaza namba yako ya simu unayotumia ya ukweli na uwe umejiunga na huduma za mitandao kama Tigopesa,m pesa au airtel money. Kumbuka baada ya kujaza fomu unatakiwa kuilipia fomu Tshs. 15,000 Ada ya uanachama Tshs. 15,000 pamoja na Akiba ya uwekezaji Tshs. 7,000 jumla unatakiwa kulipia Tshs. 37,000 elfu thelathini na saba na utalipia kwa njia ya mobile banking kupitia Airtel money katika namba ya Muweka hadhina ANTHONY LUCAS namba ya malipo 0686 95 72 33 ila kama unatumia mitandao tufauti na airtel unaweza pia ukalipa ada kupitia huo huo mtandao wako kwa kuja airtel money tutaipokea..

Kujiunga ni rahisi bofya katika Link ifuatayo hapa chini imeandikwa “FOMU YA KUJIUNGA” jaza fomu ya kujiunga na uanachama ili upate mkopo nafuu usiokua na riba! Jaza fomu kisha lipia ada ya Uanachama Tshs.37,000!! BOFYA KATIKA LINK IFUATAYO YENYE RANGI YA BLUE HAPA CHINI UJAZE FOMU