Klabu ya Leicester City wamepoteza nafasi ya kufungua mwanya wa alama tano kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutoka sare 2-2 na West Brom.
Salomon Rondon alimkwepa Robert Huth na kuwapa West Brom uongozi dakika ya 11 lakini Danny Drinkwater alisawazishia Leicester.
Andy King aliwaweka Leicester uongozini lakini Craig Gardner alisawazishia West Brom kupitia mkwaju wa adhabu.
Leicester waligonga mwamba mara mbili katika mechi hiyo iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium, lakini hawakubahatika kupata bao la ushindi.
Sare hiyo imewaacha Leicester alama tatu pekee mbele ya Tottenham Hostspur.
Spurs wanaweza kwenda kileleni iwapo watafanikiwa kuwashinda West Ham uwanjani Upton Park Jumatano.
Leciester wamo alama sita mbele ya Arsenal ambao watakutana na Swansea leo Jumatano.
West Brom, ambao sasa wameshindwa mechi mbili pekee kati ya 10 walizocheza majuzi zaidi ligini wamo nambari 13 ligini, alama 12 kutoka eneo la kushushwa ngazi.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa Jumanne
• Aston Villa 1-3 Everton
• Bournemouth 2-0 Southampton
• Leicester 2-2 West Brom
• Norwich 1-2 Chelsea
• Sunderland 2-2 Crystal Palace