Mastaa wa Real Madrid Wawachapa Wenzao wa Tanzania

Mastaa wa Real Madrid Wawachapa Wenzao wa Tanzania

Mastaa wa Real Madrid Wawachapa Wenzao wa Tanzania

MASTAA wa zamani wa timu ya Real Madrid leo wamewafunga mastaa wenzao waliowika hapo nyumba wa Tanzania mabao 3 kwa moja katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mastaa wa Real Madrid wakiongozwa na nguli wa mchezo huo wa mpira wa miguu Luis Figo walifanikiwa kuwafunga mastaa wa Tanzania baada ya mpambano mkali ambao ulikuwa na mvuto muda wote wa mchezo.

Hadi nusu ya kwanza ya mchezo inamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa sawa kwa magoli (1-1). Mastaa wa Real Madrid walionekana kuwa na kiu zaidi ya magoli katika kipindi cha pili ambapo walifanikiwa kupata goli la pili. Hadi kipenga cha mwisho kikipulizwa mastaa wa Real Madrid 3 na mastaa wa Tanzania wakiambulia bao moja.