Mashindano ya Soka kwa Vijana Taifa Kufanyika Mwanza, Makocha 32 Kunolewa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
 
MASHINDANO ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yatafanyika Desemba mwaka huu jijini Mwanza. Akizungumza wakati wa kutangaza mpango wa programu ya vijana inayolenga Fainali za Afrika za U17 mwaka 2019 ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote.
 
Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh. milioni 350. Rais Malinzi aliwashukuru wakurugenzi wa shule za Alliance (James Bwire) na Lord Baden Powell (Kanali mstaafu Idd Kipingu) kwa kukubali shule zao kuwa za kwanza kuanzia programu hiyo ya vijana.
 
Pia aliishukuru kampuni ya Symbion ambayo imetoa sh. milioni 100 kwa ajili ya kuunga mkono mashindano hayo ya U12. Symbion ni moja ya wadau wanaoshirikiana na TFF katika mpango wa miaka mitano ya programu za vijana. Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo ambayo imeambatanishwa (attached).

MAKOCHA 32 KUHUDHURIA KOZI YA OLIMPIKI
Makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watahudhuria kocha ya ukocha ya ngazi pevu (advance) iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 13 mwaka huu.
 
Kozi hiyo itakayomalizika Oktoba 25 mwaka huu itaendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulrich Marriot kutoka Shelisheli, na makocha wanatakiwa kuripoti hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Oktoba 12 mwaka huu jioni.
 
Makocha hao ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).
 
Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
 
Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).
Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za ukocha za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).   
BONIFACE WAMBURA, MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA