Mashindano ya Ngumi Taifa Yakosa Udhamini Dar

Mchezo wa Ngumi Tanzania

Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa Ngumi wa Timu ya Ashanti ya Mkoa wa ILala kimichezo, Rajabu Mhamila amesikitishwa na kitendo cha Mashindano ya Taifa ya mchezo wa ngumi kukosa mdhamini hata mmoja ilhali kuna wadhamini wengine wamekuwa wakidhamini hata mashindano ya mbio za mbuzi.

Akizungumza leo wakati wa mashindano hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam na kushirikisha mikoa 18 yalioanza tangu Jumatatu, amesema nasikitika mikoa karibia yote ya Tanzania Bara kukosa wadhamini wakati makampuni yangeweza kutumia fursa hiyo kujitangaza.

Alisema wadhamini wamekuwa wakigombania nafasi ya udhamini katika mchezo mmoja tu wa mpira wa miguu huku wakigoma kusaidia kuiinua michezo mingine ukiwemo wa ngumi, licha ya kupelekewa barua za maombi ya udhamini.

“Ufadhili basi upatikane mdogo…nasikitika mpaka sasa mashindano yapoendelea hakuna hata zawadi za mshindi ukiangalia mabondia wengi kutoka mikoani wamekuja kwa gharama zao kwa kila kitu ikiwemo usafiri, maradhi na mahitaji mengine. Yaani hata timu hizi zikishinda hawana cha kupewa kama kumbukumbu wanaporudi mikoani mwao hii ni aibu,” alisema Mhamila.

“Inasikitisha sana nchi yenye rasilimali tele lakini watu wengi wanashindwa kusaidia mchezo wa ngumi tena wa taifa, bali wamekuwa wakitoa sapoti katika mambo mengine ambayo hayana hata mwelekeo ikiwemo michezo kazaa ambayo aina hata vyama kama mbio za mbwa na mbuzi ilhali michezo hiyo aina hata vyama kama ilivyo BFT.

Alisema Katibu Mkuu wa BFT, Makore mashaga alipepeka maombi mbalimbali ya udhamini wa mashindano ya ngumi ya taifa karibuni kwa makampuni 30 nchini lakini amekosa ufadhili wa aina yoyote hata maji ya kunywa kwa wachezaji wawapo ulingoni.