Mashindano ya KCB East African Tour 2011 yazinduliwa

Mwenyekiti wa Mchezo wa Golf Arusha 'Gymkana Club', Richard Gomes akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano ya KCB East African Tour 2011.

Na Janeth Mushi
Arusha

MASHINDANO ya Benki ya Biashara Kenya (KCB) East Africa Golf Tour 2011 yanayoanza leo mjini hapa katika viwanja vya Arusha Gymkana Club, mshindi wa mashindano hayo anatarajia kujinyakulia kitita cha sh. 3,630,000 fedha za Kitanzania.

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo yanatotarajiwa kufikia tamati Jumamosi hii.

Alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji vya wachezaji ndani ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni pamoja na kuitangaza benki hiyo.

Manyenye aliongeza kuwa kwa mwaka huu mashindano hayo yameshafanyika katika klabu tatu, ambazo ni Thika Golf klabu, Muthanga, Nyanza na sasa ambayo yanafanyika katika viwanja vya Gymkana.

“Tumeanza kuwekeza katika mchezo wa gofu kisha tutaanza kuwekeza katika mpira wa miguu kwa kuwa wadhamini kwani kuna baadhi ya wadhamini ambao wamekuwa wakidhamini kwa muda mrefu, kwa hiyo wakitoka nasi tutaanza kudhamini mchezo huo unaokua katika nchi yetu,” alisema Manyenye.

Pichani ni juu ni; Mwenyekiti wa mchezo wa Golf wa Mkoa wa Arusha Gymkana Club, Richard Gomes akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shughuli za uzinduzi wa mashindano ya KCB East African Tour 2011, mashindano yanayotarajiwa kuanza leo katika viwanja vya Gymkana mjini Arusha (Picha na Janeth Mushi-Arusha)