Mashindano Mbio za Mashua ‘Mercedes Benz Cup 2015’ Yafanyika

Washiriki wakipambana na mawimbi wakati wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar.

Washiriki wakipambana na mawimbi wakati wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar.

DSC_0159

Mashua zenye tanga zinazojaza upepo zikichanja mbuga katika mawimbi makali kwenye bahari ya hindi kwenye fukwe za Yatch Club wakati wa mashindano ya mbio za Mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyodhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors kwa miaka 9 sasa, yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu

KLABU ya Yatch ya Dar es salaam iliyopo Msasani jijini Dar es salaam inatafuta fedha kuwezesha washiriki wake wanne katika mbio za mashua za kisasa kwenda kushiriki michezo ya All Africa games itakayofanyika baadae mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa patashika ya siku mbili ya mbio za mashua za kisasa zinazosukumwa na matanga yanayopokea upepo na zile ambazo hazina.

Mbio hizo ambazo zimedhaminiwa na CFAO Motors kupitia bidhaa yake ya Mercedes Benz Cup 2015 zilishirikisha watu 30 wakiwa ndani ya mashua 15 za aina tofauti.

Ofisa mmoja wa klabu hiyo Andrew Bogd alisema kwamba ushiriki wa watanzania katika mashindano ya kimataifa hautakuwa wa kwanza kwani wameshashiriki katika mchezo hiyo Afrika Kusini na Morocco mwaka jana.

Alikuwa akizungumzia mafanikio ya klabu hiyo katika kuufanya mchezo huo kujulikana kwa wazawa wa Tanzania ambao wanapenda michezo ya katika maji hasa ya kukimbiza mashua.

Katika mbio hizo ambapo kulikuwa na washindi takribani zaidi ya saba kwa kuzingatia daraja mshindi wa mashua zenye tanga inayojaza upepo alikuwa Al Bush akishirikiana na Robert Fine. Mshindi wa Pili wa ngazi hiyo alikuwa Michael Sulzer aliyekuwa katika mashua na Andreas Schmidt na ushindi wa tatu ulikwenda Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren.

 

Washindi hao walikabidhiwa tuzo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin ambaye safari hii katika udhamini wao walikuwa wanatangaza gari la Mercedes GL –CLASS.

Washindi wengine katika kategori ya mashua za kisasa za kawaida walikuwa Andrew Boyd akiwa na Max Pennan Kok wakati washindi wa pili walikuwa David Scott akiwa na Cassie Dietliefs na washindi wa tatu walikuwa Cyrille Girardin na Gemma Quickenden.

Mercedes Benz ambao wanadhamini mashindano mbalimbali ya mashua za kisasa za ngazi mbalimbali duniani, wamekuwa wakidhamini michuano hiyo ya Dar es salaam kwa mara ya 9 sasa.

Msemaji wa Yatch Club, Bogd akizungumzia michuano hiyo iliyokuwa ya siku mbili alisema iliyiojaa changamoto kubwa hasa siku ya kwanza ambapo mabahari walioonesha umahiri kukabiliana na upepo mkali na kuongoza mashua zao katika muda waliopaswa kuufikia wakishindana katika mfumo wa juu hadi chini au kwenda kwa mfumo wa pembetatu.

Siku ya kwanza ya mbio hizo Jumamosi upepo ulivuma kwa kasi ya noti 20 kwa saa.

“ …haikuwa kazi rahisi siku ya kwanza. Lakini hiyo ndio raha ya mchezo huu.Bahari inapokuwa ‘ngumu’ ambapo waendesha mashua hao ni kama vile wanataka kutemwa kutoka kwenye mashua, hivyo wakilazimika kutumia maarifa yao kuidhibiti, ndio raha ya mchexzo wenywe” alisema Bogd.

 

1st spinnaker boat - Al Bush and Robert Fine

Mshindi wa mashua zenye tanga inayojaza upepo Al Bush akishirikiana na Robert Fine wakirejea katika fukwe za Yatch Club jijini Dar es Salaam wakati wa mashindano hayo ya mbio za Mashua za Mercedes Benz yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors kupitia bidhaa ya Mercedes Benz Cup 2015 mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.

Washiriki walilazimika kufanya hatua saba za mbio hizo ambapo kila hatua ilikuwa ni dakika 40.

Pamoja na washiriki hao kupewa zawadi ofisa huyo alitaka watu zaidi kushiriki katika mashindano hayo ambayo kwa jinsi siku zinavyoenda watanzania wengi zaidi wanafika kujifunza mashindano hayo ambayo yanahitaji maarifa na pia kuzingatia usalama kwa kutumia mashua za kisasa za aina tofauti.

Katika mashindano hayo huwa kunakuwa na mashua kubwa na nyingine za kati na ndogo.

Aidha alisema kwamba wanaanzaa kufundisha mchezo huo kuanzia miaka minane na kwamba huwezi kufundisha udhibtii wa mashua kwa mtu mzima kwani kuna hatua mbalimbali zinazojenga uzoefu wa mchezo wenyewe.

Alisema watoto ambao sasa wameshapita umri wa kuendesha mashua za kati wameshaanza kushiriki na kwamba wanatoa changamoto kubwa kwa washiriki wenye umri mkubwa katika mchezo huo.

Dar es Salaam Yacht Club ambayo hufanya mashindano ya mashua ya kisasa zikiwemo catamaran, Cadets, yachts na Lasers ilianzishwa mwaka 1933 katika bandari ya Dar es salaam, mwaka 1967 ilihamishiwa ilipo sasa la Leopard’s Cove, ghuba ya Msasani.

Panmoja na kufanya shughuli za mbio za mashua pia wana bwawa la kuogelea, baa na mgahawa.

IMG_2786

Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin aliyeipa mgongo ‘camera’ akijaliana jambo na Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (aliyesimama kushoto katikati) pamoja na Meneja Masoko wa CFAO Motors, Shekha Said. Wengine ni maofisa wa Yatch Club jijini Dar, kabla ya zoezi la kukabidhi vikombe na zawadi kwa washiriki.

Spinnaker Winners, Al Bush and Robert Fine

Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto) akikabidhi kikombe kwa washindi wa kwanza wa mashindano ya Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush aliyeshirikiana na Robert Fine, huku Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani akishuhudia tukio hilo.

MercedesCupWinners, Al Bush and Robert Fine with Andrew Boyd and Max Pennan Kok

Washindi wa Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush, Robert Fine waliosindikizwa na Andrew Boyd wa Yatch Clup (wa pili kushoto) pamoja na Max Pennan Kok wakifurahia kikombe chao katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto) na Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia).

IMG_2908

Washindi wa Mercedes Benz Cup 2015, Al Bush, Robert Fine katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin (kushoto), Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (wa tatu kulia), Meneja Masoko wa CFFAO Motors, Shekha Said (wa pili kulia) pamoja na Meneja Mauzo wa matairi CFAO Motors, Pietre Van Eeden (kulia).

Spinnaker Runner Up Michael Sulzer

Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Eric Potin akimpongeza mchezaji wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015, Michael Sulzer kwa ushiriki wake.

Non-Spinnaker Runners Up David Scott and Casey Dietliefs

Mshindi mdogo kuliko wote wa mashua za kawaida shindano la Mercedes Benz Cup 2015, Casey Dietliefs (katikati) aliyeshirikiana na David Scott (kushoto) wakipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia).

DYC Commodore Brian Grant and CFAO Aldo Pangani

Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani (kulia) akisaidiwa na Mwenyekiti wa Dar Yatch Club, Brian Grant wakati akikata utepe kuzindua gari iliyotolewa na kampuni ya CFAO Motors kwa Dar Yatch Club kama shukrani ya ushirikiano baina ya CFAO Motors na Dar Yatch Club.

IMG_2839

Mkurugenzi wa fedha wa CFAO Motors, Aldo Pagani na Meneja Masoko wa CFAO Motors, kwa pamoja wakizindua gari hiyo wakati wa mashindano ya Mercedes Benz Cup 2015.

DYC Commodore Brian Grant

Mwenyekiti wa Dar Yatch Club, Brian Grant akiwasha gari hiyo kuashiria uzinduzi rasmi.

IMG_2804

Mmoja wa wananchama wa Yatch Club akiangalia gari aina ya Mercedes Benz GL Class iliyowekwa katika viwanja vya Yatch Club kama nembo ya udhamini wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz.

IMG_2823

Pichani juu na chini ni washiriki wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz na familia zao wakisubiri zoezi la kukabidhiwa zawadi na vikombe kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo CFAO Motors mwishoni mwa juma.

IMG_2824

 

IMG_2913

Washiriki wa mashindano ya mashua ya Mercedes Benz Cup 2015 katika picha ya pamoja.