Wayne Rooney alifunga bao lake la kwanza katika uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005 na kuiwezesha timu yake kupanda katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Liverpool ilitawala mchezo huo huku mkwaju wa Emre Can ukipanguliwa na kipa David De Gea. Lakini Liverpool walilazimika kulipa makosa yao wakati Wayne Rooney alipofunga mkwaju mzuri akiwa karibu na eneo la hatari baada ya kichwa cha Marouane Fellaini kugonga mwamba wa goli.
Manchester United ambao sasa wako katika nafasi ya tano walikuwa hawajashambulia hata mkwaju mmoja katika lango la Liverpool hadi mshambuliaji huyo wa Uingereza alipofunga bao hilo la ushindi.
Liverpool imebaki katika nafasi ya tisa ikiwa alama sita nyuma ya Manchester United
Nayo Arsenal ilibanwa mbavu na wenyeji wao timu ya Stoke City baada ya kumaliza dakika 90 bila ya kufunga na hivyo Arsenal ikipanda ena kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi 44 sawa na Leicester City huku Manchester City akiwa nafasi ya tatu na pointi zao 43, na kuendelea kuleta ushindani wa ligi hiyo