Mashindano ya Olimpiki mjini Rio kufunguliwa rasmi kesho Ijumaa, lakini hali bado haijakaa vizuri katika mazingira ya michezo hiyo. Vilabu mbali mbali barani Ulaya vinajiweka tayari kwa msimu ujao
yamebakia masaa tu hadi kuanza rasmi michezo ya 31 ya Olimpiki mjini Rio. Mahakama ya kimataifa ya michezo inachukua hatua za haraka kuamua rufaa zilizopelekwa katika mahakama hiyo na wanariadha wa Urusi kupinga zuio lao kushiriki michezo ya Rio ambapo sherehe za ufunguzi zinatarajiwa kufanyika mapema.
hatua ya kuzuiwa kwa njia mpya ya treni kwa ajili ya eneo la michezo hiyo ya Olimpiki ni moja katika ya changamoto zilizowakabili watayarishaji wa michezo hiyo pamoja na kuweza kuweka viwanja pamoja na vifaa kuwa tayari kwa ajili ya michezo hiyo.
Wanamichezo kadhaa wa Urusi wamepeleka katika mahakama hiyo rufaa ya kutaka kuruhusiwa kushiriki katika michezo hiyo baada ya shirika linalopambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu misuli, doping kugundua kuwa kulikuwa na utaratibu wa kitaifa kuwapa wanamichezo wa nchi hiyo dawa hizo.