Na Kibada Ernest Kibada –Katavi.
Mkoa wa Katavi umezindua mradi wa huduma ya uzazi wa Mpango unayotolewa bure na Marie Stopes Tanzania (MST) kwa Wananchi wa Mkoa huo.
Uzinduzi huo ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima kwa niaba ya Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi na kuhudhuriwa na na wakazi wa Mkoa wa Katavi uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili ulioko Mjini Mpanda.
Dkt Msengi katika hotuba yake alisema kuwa uzazi wa mpango ni hiari ambao mtu au wanandoa wanaamua idadi ya watoto watakao zaa kwa mpangilio uliokubalika kwa ajiri ya afya zao
Alisema huduma hiyo ya mpango wa uzazi iliyozinduliwa katika Mkoa wa Katavi mpango huo utasaidia kupunguza vifo vya akina Mama na watoto katika Mkoa wa Katavi na watoto chini ya umri wa miaka mitano ikiwa ni katika kutimiza malengo ya milenia namba nne na namba tano
Alifafanua zaidi ya wanawake elfu nane hufa hapa nchini kila mwaka kutokana na uzazi na kinachoshangaza wanawake walioolewa ndio wengi wao wamekuwa wanashindwa kupata huduma ya uzazi wa mpango
Alisema wananchi wa Mkoa wa Katavi watumie fursa hiyo kuwahamsisha watu watumie njia za uzazi wa mpango kwani ni salama
Dr Msengi aliwataka wananchi wawatumie wataalamu ili waweze kuwapatia ushauri na kuwaelimisha umuhimu wa uzazi wa mpango na kuwapuuza watu ambao wanatafsiri vibaya huduma ya mpango wa uzazi na wanaopinga uzazi wa mpango
Aliisema kumekuwepo na imani potofu na taarifa zisizo sahihi kuhusu uzazi wa mpango ambazo zimesababisha kina mama wengi kuwa waoga wa kutumia njia hizo na kishia kushika mimba zisizotarajiwa
Kwa wanaume njia ya za uzazi wa mpango ni chache kwa hiyo fursa ya kushiriki ni ndogo ukilinganisha na wanawake hata hivyo kuna baadhi ya wanaume huwazuia wake zao kutumia uzazi wa mpango kufanya hivyo ni kutomtendea haki mwanamke
Alisema wanaume wamekuwa wakidhani kuwa jukumu la kunga kizazi na mpango wa uzazi ni kwa ajiri ya mwanamke tuu wakati jukumu hilo ni la mwanaume na mwanamke hivyo huduma hiyo waakikishe inawafikia wananchi wote wa Mkoa wa Katavi hata yale maeneo ambayo yamekuwa yakifikika kwa shida kama vile Ilunde Bugwe, Mnyagala ambako unakuta mtu mmoja anakuwa na watoto 40 wa kuzaa mwenyewe na wake zaidi ya watatu
Nae Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Marie Stopes Tanzania Eliy Reweta alisema pamoja na kuendeleza kazi zilizokuwa huko nyuma timu za utoaji huduma zimeongezwa katika mikoa ya Singida , Kilimanjaro ,Manyara na Katavi lengo ni kumfanya kila mtu achague njia ya uzazi ya mpango anayohitaji
Alisema huduma zinazo tolewa kupitia shirika la Marie Stopes Tanzania zinachangia asilimia ishirini na tano yahuduma zote za mpango wa uzazi ukiondoa kondomu
Alifafanua kuwa huduma ya uzazi wa mpango hutolewa na timu ya wataalamu wa uzazi wa mpango waliopitia mafunzo maalumu na kila timu inagari linalozunguka na kutowa huduma hizo katika Zahanati na vituo vya afya vilivyoko katika maeneo ya vijijini kwa siku 21 kila mwezi
Nandio maana kwa kutambua umuhimi huo Marie Stopes imekabidhi gari jipya wakati wa uzinduzi huo kwa ajiri ya Mkoa wa Katavi litakalo saidia kutowa huduma na kuwafikia kila mtu mahari pale alipo alisema Elly
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa alieleza kuwa mpango huo utasaidia kuwafanya watu waweze kuwa na utatatibu mzuri wa kuzaa watoto kwa mpangilio kuliko iliyo sasa
Alisema Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa miwili inayoongoza kwa kuwa na ongezeko kubwa la watu ikiwa inaufuatia Mkoa wa Dares salaam
Kwa upande wake mrembo wa mashindano ya Miss Marie Stopes Tanzania Doreen Benne alisema kuwa uzazi wa mpango unamkinga mtu kupata mimba zisizotarajiwa na kumwepusha na kuingia kwenye mtego wa kutoa mimba kusiko salama
Pia wanawake wengi kwa sasa kupitia mpango huo wa uzazi wanafanikiwa kumaliza masomo yao na kutengeneza maisha kabla ya kuanza mpango wa kutengeneza familia