Marekani Yaondoa Wafanyakazi wake Bangui

SERIKALI ya Marekani, imesema imewaondoa raia wake katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema haijavunja uhusiano wake wa kibalozi na serikali ya nchi hiyo, ila imechukua tahadhari kuhusu usalama wa raia wake.

Marekani pia imeonya raia wake dhidi ya kwenda nchini CAR wakati wa machafuko hayo.

Hali ya wasi wasi imetanda katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, Bangui, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kufika mji huo.

Mjumbe mmoja wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kuwa ameshuhudia raia wa mji huo wakiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na na tishio la shambulio.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umewahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo, nayo serikali ya Marekani imetoa wito kwa raia wao kuondoka nchini humo.

Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeagiza usalama kuimarisha katika ubalozi wake mjini Bangui, baada ya kushambuliwa na waandamanaji.
Wanajeshi wa Serikali ya CAR

Wanajeshi wa Serikali ya CAR

Waandamanaji hao walirusha mare ya kuchoma bendera ya Ufaransa.

Raia hao wanataka serikali ya Ufaransa kusiadia kuzima uasi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanadai serikali ya Ufaransa imewatekeleza.

Ufaransa ina takriban wanajeshi mia mbili mjini Banguia na utawala wa nchi hiyo umetoa wito kwa Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kukabiliana na wanajeshi wa waasi ambao wameuteka maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo.

Lakini rais wa Ufaransa Francois Hollande amekataa wito huo.

-BBC