Kipa Aliyezitumkikia Klabu za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti na sasa Azam FC, Ivo Mapunda ameeleza kuwa bado ana kiu ya kucheza soka la kulipwa.
Mpunda, amepanga kutumia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) kwa ajili ya kujitangaza kimataifa ili apate nafasi ya kucheza soka la kulipwa.
Kipa huyo, alijiunga na Azam FC kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Simba inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Ujio wake kipa huyo kwenye kikosi cha Azam, utaongeza ushindani kwa makipa wa timu hiyo aliowakuta ambao ni Aishi Manula na Mwadini Ally.
Ameongza kuwa ana misimu miwili hajacheza michuano ya kimataifa akiwa Simba, hivyo amepanga kuitumia kwa ajili kujitengenezea soka kwenye klabu za nje ya nchi.
Amesema, kwa kuwa michuano hiyo inashirikisha klabu kubwa hivyo anaamini kama akiitumia vizuri, basi kuna uwezekano wa kupata dili la kwenda kucheza nje ya nchi kutokana na uwezo wake mkubwa alionao wa kuokoa michomo golini.