Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.
Dk. Asha Rose Migiro akiendelea kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
Dk. Asha Rose Migiro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na siasa kwa sasa. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
Dk. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
Dk. Asha Rose-Migiro (katikati) akizungumza jambo Waziri Membe sambamba na Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberi Kacou (kushoto) waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji akimpongeza Dk. Asha Rose Migiro kwa kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipokutana leo katika Uwanja wa ndege.
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha ametua nchini Salama.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa.