Mapigano ya Kikabila Yaendelea Kenya

Namna majengo yalivyo athirika na mapigano

WATU 11 wameuawa na wengine 15 kujeruhiswa mapema Alhamisi kwenye shambulio la kulipiza kisasi baina ya jamii mbili zinazohasimiana katika eneo la Tana River Delta. Shambulio linaifikisha 22 idadi ya watu waliouawa kwenye mapigano hayo ya kikabila yaliyozuka upya jana katika eneo la Nduru.

Shambulio hili la alfijiri limetekelezwa katika kijiji cha Kibisu hatua chache tu kutoka eneno la Nduru kulikouawa watu wengine 10 jana. Wenyeji wa kijiji cha Kibisu wanasema kuwa, kundi la wavamizi waliofunika nyuso zao, walikivamia kijiji hicho mwendo wa saa moja na nusu asubuhi na kuwakata mapanga,mishale huku wakichoma nyumba zao.

Miongoni mwa waliouawa ni watoto watano, wanawake watatu na wanaume watatu wawili kati yao ikiaminika kuwa miongoni wa wavamizi. Kupitia mkuu wa idara ya Polisi nchini Kenya Aggrey Adoli anasema watatu miongoni wa walaiouawa walichomwa kiasi cha kutambulikana ndani ya nyumba zao. “Kulitokea uvamizi katika eneo la eneo Delta, na miongoni mwa waliouawa kwenye uvamizi huo wanashukiwa wa uvamizi”alisema Bw Adoili.

Shirika la Msalaba mwekundi linasema kuwa zaidi ya majeruhi 13 wamesafirishwa hadi hospitali za wilaya ya Malindi kwa matibabu ingawa wanasema kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Hali ya wasi wasi inazidi kutanda katika eneo Tana Delta, huku mauaji hayo yakisalia kuwa kitendawili sio tu kwa wenyeji ambao ni jamii hizi mbili hamisimu zinazoishi katika eneo hilo, bali kwa taifa zima kwa jumla. Jamii ya Wapokomo ambayo ni Wakulima katika eneo hilo la Tana Delta, inalaumiwa kwa kuteleleza mauaji dhidi ya majirani zao Wa Orma ambao wanazingatia zaidi utamaduni wa ufugaji wa kuhama hama.

Mauaji ya Tana Delta yanazidi kupamba moto hata baada ya serikali kutuma vikosi vya jeshi la Usalama katika eneo hilo na Bw Adoli alisema kuwa ni dhahiri visa hivi vya mauaji vinafadhiliwa na watu wenye ushawishi na uwezo mkubwa.

“Tungependa kuwaomba wenyeji wanaotusaidia kuwasaka wavamizi msituni wasiende msituni na sialha kuwaua wavamizi, ili tuweza kupata ushahidi ya ni nani anayewatumia, kama ni wafanyi biashara au wanasiasa ili tupate ukweli na kina cha maneno haya” aliongeza Adoli. Zaidi ya watu 200 wameuliwa wilayani Tana River tangu mapigano hayo yazuka mwezi Agosti mwaka uliopita hatua iliyosababisha serikali kutuma kikosi GSU wasiopungua 2000 mbali na hatua ya Rais Kibaki kutangaza amri ya kutotoka nje katika eneo hilo.

Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binaadamu yamewanyoshea kidole cha lawama wanasiasa katika eneo hilo ambao wanaaminika kuchochea ghasia hizo. Baadhi ya wachambuzi wanasema wanahofu ya kukubwa na ghasia uchaguzi wa Kenya unaotarajiwa kufanyika mwezi machi mwaka huu. Ni takriban chini ya miezi miwili kabla ya kufanyika uchaguzi huo ambao utakuwa wa kwanza tangu kutokea ghasia za baada ya uchaguzi miaka mitano iliopita ambapo zaidi ya watu 1000 waliuwawa huku wengine zaidi ya laki sita wakiachwa bila makao.

Kenya ilio na idadi ya watu milioni 40, ni milioni 14 pekee waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao. Nchi hiyo pia kwa sasa inakabiliwa na changamoto kubwa katika sekta ya usalama hasaa baada ya kundi la Al shabaab kutoa vitisho vya mara kwa mara kuishambulia Kenya hadi pale itakapotoa vikosi vyake nchini Somalia vinavyowasaka al shabaab wanaoaminika kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la al qaida.