Maonyesho ya Nane Nane Dodoma!

 

 Afisa habari na uhusiano wa  Mfuko wa Pensheni (PPF) Edwin Kyungu akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Shule ya Sekondari Wella ya Mjini Dodoma kuhusu huduma mbalimbali za mfuko huo jana mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma.

Mhadhiri katika Chuo cha Mipango Dodoma Emmanuel Nyankweli akiwaeleza wanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Wella mjini Dodoma jana wakati walipotembelea banda la Wizara ya fedha juu ya taratibu na sifa za kujiunga na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayofanyika mkoani Dodoma kitaifa.

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Mipango Dodoma Bartazar Ngeze akiwaeleza wananchi mbalimbali waliotembelea banda la Wizara ya Fedha juu ya taratibu mbalimbali za kujiunga na Chuo hicho katika maonyesho ya wakulima yanayoendelea mjini Dodoma. 
Meneja wa Mfuko wa Pensheni(PPF) wa Kanda ya Mashariki na Kati Anthony Ndadavala akimweleza mmoja wa wakazi wa Dodoma shughuli mbalimbali za mfuko na faida yake jana mkazi huyo alipotembelea banda la Wizara ya fedha wakati wa monyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea.
 
Afisa uendeshaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma(PSPF)  Francis Mselemu  akitoa maelezo jana kwa Assistant Inspekta wa Polisi Juma Seif  Abdallah na Sajenti Noel Marko Nkumbi juu ya huduma za mfuko huo kwa watumishi wa umma wanapostaafu utumishi wa umma. Afisa huyo alitoa maelezo hayo wakati Polisi hao walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma(PSPF)  Fatma Elhady akitoa ufafanuzi kwa Inspekta J. Mwinyi jana juu ya mafao ya wastaafu wakati maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea mjini Dodoma.