Maoni ya Mbunge John Mnyika Kuelekea Digitali

Mbunge John Mnyika


MAONI majibu yenu kwa kuzingatia kuwa kazi ya wabunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali: baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa kuhama kutoka analojia kwenda digiti kwa mkoa wa Dar es salaam; kwa watumiaji, nini faida na athari mlioanza kuzipata kwa wenye ving’amuzi?

Na nini kikwazo kwa wengine ambao hamjahamia mpaka sasa? Na nini mnataka watoa huduma na mamlaka zingine kuzingatia? Katika hatua ya sasa, ni muhimu Tanzania Consumer Advocacy Society (TCAS) ifanye tathmini ya kina kwa niaba ya watumiaji kwa ajili ya hatua zake.

Ikumbukwe kwamba Consumer Federation of Kenya ilikwenda mahakamani na kuzuia mitambo kuzimwa watumiaji tarehe 31 Disemba 2012, na mahakama imesitisha mpaka itakapofanya uamuzi wake wa msingi.

Kwa upande mwingine, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC) litumie mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu cha 37 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano namba 12 ya mwaka 2003 na vifungu vingine vinavyohusika kushughulikia malalamiko yaliyotolewa kwa nyakati mbalimbali kwa kuzingatia tahadhari tuliyotoa kwa serikali bungeni miezi mingi iliyopita kuhusu athari zitazojitokeza kwa kutozingatiwa kwa maandalizi muhimu.