Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Maonesho ya Miaka 50 ya Ikulu na kushoto ni Mke wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere, kulia ni aliyeshika sahani ni Ened Munthali Mkuu wa Sehemu ya Mipango Ikulu. Maonesho hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dares Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani akiwa na Mke wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere wakati akielekea sehemu maalum ya kuzindua Maonesho ya Miaka 50 ya – Ikulu yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo wanne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi mbalimbali wa nchi za nje na wawakilishi wa ofisi za balozi hizo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya jumla ya Bajeti ya Serikali ya Tanzania unaoendelea katika ukumbi wa mkutano wa Ubungo- Plaza jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO – MAELEZO)