Na Woinde Shizza, Arusha
WACHIMBAJI wa madini ya vito nchini wametakiwa kushiriki katika maonyesho ya wachimbaji wadogo wa madini ili kuweza kutumia fursa hiyo ya kuuza na kupanua wigo wa kupata masoko ya ndani na nje ili kuweza kukuza uchumi wao na pato la taaifa.
Hayo yameelezwa leo na kamishina wa madini kanda ya kaskazini Elius Kayandabila wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza kesho march 9 hadi kumi katika mji mdogo wa mererani uliopo mkoani Manyara.
Hata hivyo amesema kuwa lengo haswa ni kuonyesha madini hayo ya wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo kuwakutanisha na wafanyabiashara wakubwa wa ndani ya nchi ambapo maonyesho hayo yatawasaidia pia kupata masoko kwa urasi.
Aidha ameongeza kuwa wachimbaji zaidi ya 50 watashiriki maonyesho hayo ya madini katika mji mdogo wa marerani ambapo hii ni kwa mara ya kwanza maonyesho hayo kufanyika eneo hilo, ambapo alifafanua kuwa maonyesho haya pia ni moja ya maandalizi ya maonyesho makubwa ya kimataifa ya vito na madini ambayo hufanyika kila mwaka mjini Arusha.
Kayanda bila aliwataka wachimbaji hao kuweza kutumia fursa hiyo ya maonyesho haya ili kuweza kujifunza na kupata masoko ya ndani na nje kwa uhakika huku akiwasihi wakazi wa jiji la arusha pamoja na mkoa wa manyara kujitokeza kwa wingi kuangalia aina mbalimbali za madini zinazopatikana hapa nchini.
Aidha pia alitumia fursa hiyo kuwasihi wafanya biashara wadogo na wakubwa ambao wanafanya biashara ya madini kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya ili kuweza kupata madini hayo kwa bei nafuu na kuweza kufaamiana zaidi na wachimbaji wadogo pamoja na wafanyabiashara wadogo wa madini.