![Baadhi ya maofisa habari. elimu na uhusiano wa Serikali wakiwa Serengeti](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/06/no-1.jpg)
Baadhi ya maofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili kwenye lango la kuingia hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhamasisha utalii wa ndani nchini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
![Wanyama aina ya nyumbu mbugani Serengeti](http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/06/Pno-5.jpg)
Kundi kubwa la Nyumbu wakiwa katikati ya Barabara ndani ya hifadhi hiyo na kuufanya msafara wa magari yaliyowabeba maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali kwenda kwa mwendo wa polepole. Kwa mujibu wa taratibu za hifadhi ni kosa kwa dereva kupiga honi, kuendesha gari kwa mwendo kasi au kupiga honi ndani ya eneo la hifadhi. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.