Mzee Sumbu Galawa akimkabidhi ujumbe maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pilip Mangula, wakati yeye Wazee wenzake wa CCM kutoka mkoani Singida, Alhaji Rajabu Kundya (wapili kulia) na Mujengi Gwao (watatu kulia) walipofika Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, Januari 15, 2013, kuwasilisha ujumbe huo.
Mangula akizungumza na Wazee wa CCM kutoka mkoa wa Singida, waliofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, kumpa ujumbe maalum wa kuimarisha chama. Kushoto ni Mzee Sumbu Galawa na kulia ni Alhaj Mahami Rajabu Kundya na Mujengi Gwao. (Picha zote na Bashir Nkoromo, Uenezi-CCM)