Manchester United Yachapwa Yaondolewa, City Yasonga 16 Bora UEFA.


Michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya imeendelea tena kwa michezo kadhaa ikiwa ni hatua ya makundi kuelekea hatua ya 16 bora.

Manchester United wakicheza ugenini dhidi ya VfL Wolf-Sburg imeambulia kichapo cha mabao 3-2 na kuondolewa katika michuano hiyo, Wakati Manchester city wakiwa nyumbani dhidi Borussia Monche-ngladbach wametakata kwa ushindi wa bao 4-2 mabao ambayo yamefungwa na Jimenez Silva, Sterling pamoja na Bony Wilfried na kuwa vinara wa kundi D.

Vinara wa kundi A Timu ya Real Madrid wakiwa nyumbani Bernabeu dhidi ya Malmo kutoka Sweden Madrid wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa kishindo baada ya kuwachapa Malmo kipigo cha bao 8-0.

Mabao ambayo yamefungwa na wachezaji karim Benzema mabao (3), Christiano Rolnado mabao (4) pamoja na Mateo kovacich bao (1).

PSG ya Ufaransa wamewadhibu Shakhtar Donetsk ya Ukraine kwa kichapo cha mabao 2-0, ambayo yamefungwa na wachezaji Lucas Moura pamoja na Zlatan Ibrahimovic.

Michezo mingine PSV Eindhoven imeichapa 2 -1 CSKA Moskova , Benfica imelala kwa 1 – 2 Atl Madrid, Galatasaray imetoka sare ya bao 1 -1 na FC Astana, huku Sevilla ikishinda bao 1- 0 dhidi ya Juventusi.

Timu zilizo fanikiwa kusonga hatua ya 16 bora ni Katika kundi A ni PSG na R. Madridi, Kundi B ni VfL Wolf-Sburg na PSV Eindhoven, kundi C ni Atletico Madrid na Benifica na Man City na Benifica wakifanikiwa katika Kundi D.