Manchester United Wasaka Saini ya Cavani

edinsoncavani-cropped_1ba3aa5iee98q18z9jts8sttdwTetesi za usajili nchini uingereza zimeanzia Old Trafford ambapo ripoti kutoka klabuni hapo zinaeleza kuwa Manchester United wanamuhitaji Edinson Cavani katika Usajili wa dirisha dogo.

Tayari mazungumzo ya siri baina ya vilabu hivyo viwili tayari yameanza, huku PSG wamewaambia Manchester kuwa Mchezaji huyo Rai wa Uruguayi ataweza kuondoka klabuni hapo kwa dau la £32 million.

United miaka ya nyuma waliwahi kumfukuzia mshambuliaji huyo lakini juhudi zao zikigonga mwamba, hivyo wameamua kurudi tena kwa kasi ,ili kuweza kupata namba tisa itakayeziba pengo la Wayne Rooney ambaye inasemekana anaweza kuondoka msimu ujao.

Cavani amekuwa kwenye wakati mbaya katika klabu yake tangu kutua kwa Zlatan Ibrahimoc ambaye alisababisha kocha wa Klabu hiyo Laurent Blanc kumweka mara kwa mara Benchi huku muda mwingi akimchezesha namba ambayo hakuizoea na kumpisha Zlatan kutawala namba ambayo Cavani alijimilikisha klabuni hapo klabla ya kutua Mswideni huyo.

Cavani alitua PSG mwaka 2013 akitokea klabu ya Napoli ya Nchini Italia kwa dau la €65m, tayari ameshafunga mabao 9 hadi sasa baada ya kucheza michezo 15 msimu huu