Mamlaka ya Vitambulisho Yatimu Wafanyakazi 597

Mamlaka ya Vitambulisho Yatimu Wafanyakazi 597

Mamlaka ya Vitambulisho Yatimu Wafanyakazi 597

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA) imesitisha mikataba ya wafanyakazi wa muda 597. Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Modestus Kipilimba kwa waandishi wa habari leo Dar es Salaam, imeamua kusitisha mikataba ya wafanyakazi hao kwa kile kukosa fedha za kuwalipa kwa sasa hasa ukizingatia majukumu waliokuwa wakifanya awali yanafanywa kwenye ngazi zingine.

Alisema ktokana na kubadilika kwa mpango kazi wa NIDA ambapo kwa sasa hatua zote za usajili zinafanywa katika ngazi ya wilaya idadi ya watumishi waliopo kwa masharti ya kudumu inakidhi kukamilisha kazi iliyokusudiwa kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji na mitaa.

“…Hatua hii pia ni mwendelezo wa mpango wa mamlaka wa kurekebisha maeneo ambayo yanahitaji mabadiliko makubwa ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”, NIDA inapitia upya mikataba yote ya huduma ambayo ilifanya kwa wadau mbalimbali kujirdhisha taratibu zote za kisheria zilifuatwa na kwa ile ambayo itabainika haikufuata sheria itasitishwa mara moja,” alisema Dk. Kipilimba.