Mamlaka ya Elimu Tanzania Kukabidhi Madawati 2000

Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) Jijini Dar es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Frank Mvungi – Maelezo

MAMLAKA ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati 2,000 kwa shule za Msingi 10 zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa madawati hapa nchini. Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari Elimu na Mawasilano wa Mamlaka hiyo Bi. Sylvia Lupembe wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Wanafunzi zaidi ya 6,000 watanufaika na madawati hayo ambayo yatagharimu zaidi ya shilingi milioni mia moja na hamsini (150,000),” alisema Lupembe.

Akifafanua zaidi Bi. Lupembe alisema shule zitakazo nufaika ni Chamazi, Mbande, Boko NHC, King’ong’o, Hekima, Bwawani, Bunju, Goba, Kombo na Kingugi. Katika kuhamasisha wadau wengine kushiriki kwenye mchakato wa kuchangia madawati Bi. Lupembe alisema kuwa Mamlaka ya Elimu Tanzania imezingatia rai iliyotolewa na Waziri Mkuu ikielekeza kuwa tatizo la madawati katika shule za msingi limalizike ifikapo mwezi Juni, 2015 kwa kulipa kipaumbele suala hilo.

Pia Bi. Lupembe alibainisha kuwa tathmini ya mwaka 2013 Tanzania inaupungufu wa madawati 1,147,471 hivyo ni jukumu la kila mdau kuunga mkono juhudi hizo ili kuondoa tatizo hilo kote nchini.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB, Bi. Christina Manyenye alisema wamekuwa wakishiriki katika kuchangia mada wati ambapo kwa mwaka jana walichangia zaidi ya madawati 700.

“Tutaendelea kusaidia huduma za jamii katika maeneo mbalimbali kama tunavyofanya katika sekta ya Elimu,” alisisitiza Manyenye.

Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Mafuta ya TOTAL na wadau wengine kama Kenya Commercial Bank (KCB), na Social Action Fund wamekuwa katika ushirikiano tangu mwaka 2013 katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu hapa nchini ikiwemo ya upungufu wa madawati.