Mambo mabaya Misri; 20 wauwawa, wengine wajeruhiwa

Vurugu za waandamanaji nchini Misri

WATU 20 wameuwawa na wengine zaidi kujeruhiwa kufuatia vurugu kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Misri, katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo huku uongozi wa kijeshi ukisema kadhia hiyo haitovuruga uchaguzi.

Vikosi vya usalama vilitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi kuzuia waandamanaji waliotaka kudhibiti boma lililopo karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani. Mamia ya waandamanaji katika uwanja wa Tahrir wamekuwa wakiushinikiza utawala wa kijeshi nchini humo kuharakisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa Serikali ya kiraia.

Vurugu hizo zilianza pale ambapo polisi walipoyaondoa mahema ya kiasi ya waaandamanji 100 walioweka kambi katika uwanja huo baada ya maandamano ya ijumaa.