Mama yake Kanumba atoa wosia kwa SHIWATA

Moja ya filamu aliyocheza Steven Kanumba ijulikanayo kwa jina la Big Daddy

Na Peter Mwenda

MAMA Mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven
Kanumba amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae.

Akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na M
(SHIWATA) leo Dar es Salaam, Mama Kanumba alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mwanae kila kona ya nchi.

“Nawashukuru SHIWATA kwa moyo wa ipendo na ushirikiano mlionesha kwa familia yangu, naomba muendeleze ushirikiano mliokuwa nao wakati
mwanangu akiwa nanyi, endeleeni kushirikiana” alisema Mama Kanumba.

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji wa Kanisa la Elim
Pentekoste Ilala Bungoni, Mchungaji Livingstone Mwaitela alisema
wasanii na familia ya Kanumba wasisononeke kwa sababu Mungu alimpenda mtoto wao huyo zaidi.

Alisema wasanii waendelee kumkumbuka mwenzao kwa kubadili mambo
yasiyompendeza Mungu badala yake wajiandae kwa kufanya mambo ambayo yanampendezesha na kujiweka tayari siku akiwaita wawe tayari.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema Kanumba alikuwa mwanachama wao namba 648 akiwa mmoja wa waliojitokeza kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga nyumba za wasanii kutoka Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye kufanikiwa kupata eneo Mkuranga.

Marehemu Kanumba alifariki Aprili 5, wakati akikimbizwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka nyumbani kwake Sinza kufuatia ugomvi wa mapenzi na msanii mwenzake Elizabeth Michael (Lulu).