Mama Shujaa wa Chakula 2014 Akabidhiwa Zawadi Ukerewe

Mshindi wa Maisha Plus (Mama shujaa wa chakula) msimu wa tatu 2014, Bahati Jacob Muriga akiwa na zawadi zake.

Mshindi wa Maisha Plus (Mama shujaa wa chakula) msimu wa tatu 2014, Bahati Jacob Muriga akiwa na zawadi zake.

Baadhi ya zawadi za Mshindi wa Maisha Plus (Mama shujaa wa chakula) msimu wa tatu 2014, Bahati Jacob Muriga pichani kabla ya kukabidhiwa.

Baadhi ya zawadi za Mshindi wa Maisha Plus (Mama shujaa wa chakula) msimu wa tatu 2014, Bahati Jacob Muriga pichani kabla ya kukabidhiwa.

MSHINDI wa Maisha Plus (Mama shujaa wa chakula) msimu wa tatu 2014, Bahati Jacob Muriga hatimaye amekabidhiwa zawadi zake nyumbani kwake Ukerewe. Zawadi hizo ni pamoja na vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi milioni 20, ambapo mshindi huyo alichagua kununuliwa shamba la ekari 7, pikipiki ya magurudumu matatu aina ya Toyo, vifaa vya kilimo zikiwemo mbegu, mbolea, mipira ya kumwagilia, watering cane, pampu ya maji, pampu ya kumwagilia, koleo na dawa za kuulia wadudu na ukungu, majembe, mundu, engine oil lita 2 na petroli lita 96.

Shindano la Maisha Plus lilifikia tamati May 18, 2014 ambapo, Bahati Jacob Muriga aliibuka kidedea wa shindano hilo. Mama shujaa huyo ni mkulima kutoka Mji wa Nansio, Ukerewe Mkoa wa Mwanza na pia ni mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mhozya. Ni mjane mwenye watoto watatu na hutumia kilimo kama nguzo ya kuhakikisha mahitaji ya kifamilia yanatimizwa.

Hafla fupi ya kumkabidhi zawadi zake Bahati zilifanyika katika Ukumbi wa Afro Beach ambapo watu na wawakilishi mbalimbali kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile Kivulini, EMEDO walihudhuria ili kushuhudia jinsi anavyokabidhiwa zawadi. 

Katika hafla hiyo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe alisema viongozi wamefurahi kwa wilaya hiyo kutoa mshindi wa Mama shujaa. “..Ninayo furaha kubwa na kama kiongozi kijana kuona wilaya yetu imetoa mshindi wa shindano kubwa kama hili na kuiweka Ukerewe katika historia na ramani ya nchi…kumbe Nansio tunaweza, najisikia furaha pia kwa ushindi huu kwani toka anaanza huu mchakato wa kuchukua fomu na kuelekea Kijiji cha Maisha plus nilikua miongoni mwa niliotoa ushirikiano mkubwa kwa kutoa  ruhusa na baraka zangu za yeye kushiriki katika shindano hili,” alisema.
Aidha, mmoja wa wanafunzi wa mchezo huo Hafidhi Kunambi anayepata mafunzo ya mchezo huo ameonesha jinsi alivyojifunza namna ya kujilinda kadiri ya mafunzo aliyopata. Kwa Tanzania wanatakiwa washiriki 45 ambao wamefanya mazoezi ili kuweza kushiriki mashindano hayo kutoka maeneo mbalimbali nchini na kupata timu bora itakayoleta ushindi.