Mama Salma Kikwete Atoa Changamoto Mkutanoni New York

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika Mkutano wa kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha ulioandaliwa na Mke wa Waziri Mkuu wa Belize Mama Kim Barrow akishirikiana na Umoja wa Mataifa. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Suriname Mama Lisbeth Venetiaan na kulia ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa uliozungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York Marekani tarehe 25.9.2014. Picha zote na John Lukuwi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa. Kutoka kushoto ni Mama Kim Barrow, Mke wa Waziri Mkuu wa Belize, Mama Joyce Banda na wa kwanza kushoto ni Mama Dianne Stewart. Picha zote na John Lukuwi. 

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Joyce Banda, Rais Mstaafu wa Malawi muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi ulizungumzia namna ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York tarehe 25.9.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Sera na Mipango katika Umoja wa Mataifa Bwana John Hendra. Bwana Hendra aliwahi kuwa Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania wakati wa mkutano wa kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York tarehe 25.9.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).

Na Anna Nkinda – Maelezo, New York

NCHI za Mashariki na Kusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa fursa za elimu kwa watoto wenye umri wa kwenda shule, ubora na usahihi wa elimu, masuala mtambuka kama Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ugonjwa wa Ukimwi. Changamoto nyingine ni upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana na udahili mchache wa wasichana katika masomo ya sayansi.

Hayo yamesemwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizungumza katika majadiliano ya elimu na afya kwa vijana yaliyoandaliwa na Umoja wa kimataifa wa Taasisi za Biashara kwa ajili ya Elimu na kufanyika katika Hoteli ya Reed Smith mjini New York.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kwa upande wa sekta ya afya ina changamoto ambazo zina uhusiano mkubwa na elimu na kutoa mfano wa vifo vya akina mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi, vifo vya watoto, ndoa za utotoni, mimba katika umri mdogo, utapiamlo na upungufu wa nguvu kazi. Alisema Serikali na wananchi wa Tanzania walitambua mapema umuhimu wa kuwekeza kikamilifu katika elimu kama msingi wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia hususan lengo la pili linalohusu Elimu kwa wote.

“Serikali yetu ilianzisha  Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi na mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Mipango yote hii miwili ina malengo ya kuongeza upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote walio katika umri wa kwenda shule, kuongeza ubora na usahihi wa elimu.

Kuboresha urari wa kijinsi na walimu na ufundishaji, kuongeza tija katika uongozi na utawala bora, kurasimisha masuala mtambuka kama vile UKIMWI, Elimu ya Stadi za Maisha, elimu ya mazingira na jinsia”, alisema Mama Kikwete.

Alisema mpango wa  matokeo makubwa sasa katika elimu unalenga kujenga uwezo wa walimu kwa kutoa mafunzo ya pahala pa kazi, kusaidia watoto wasiofanya vizuri kwa kuandaa vitendea kazi mahususi vinavyozingatia umri na mahitaji, kuboresha miundo mbinu, kwa kujenga madarasa, maabara na nyumba za walimu.

Kuboresha vifaa vya ufundishaji kama vile madawati, vifaa vya maabara, kemikali na kutoa vitu vya kuongeza motisha kwa walimu. Mwenyekiti huyo wa WAMA alimalizia kwa kusema elimu bora itapatikana ikiwa afya za vijana zitaboreshwa na kuwa na mikakati ambayo inatambua uhusiano mkubwa wa masuala hayo kwani bila ya elimu timilifu ni vigumu kufikia malengo yaliyopo.

Kwa upande wake Mke wa waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mama Sara Brown ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Umoja wa kimataifa wa Taasisi za Biashara alimpongeza Mama Kikwete kwa kazi anayoifanya ya kutoa elimu kwa watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuboresha afya ya mama na mtoto.

“Nilitembelea nchini Tanzania mwaka 2007 na kujionea kazi anayoifanya Mama Kikwete nampongeza kwa hili. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu na afya bora ili waweze kuwa na maisha bora hapo baadaye,” alisema Mama Brown.

Nao wachangia mada katika mjadala huo walisema ni muhimu watoto wa kike wakapata elimu sawa na watoto wa kiume kwani wakipata elimu unyanyasaji wa kijinsia ambao unazidi kuongezeka dhidi yao utapungua na kutakuwa na usawa katika mambo mengi.

Walisema, “Wafadhili mbalimbali wamekuwa wakiwekeza katika afya na elimu hasa kwa watoto wa kike ili kuwajengea mazingira mazuri ya kusoma ikiwa ni pamoja na kuwajengea madarasa na vyoo. Ni vyema vijana wakapata elimu na afya bora ili waweze kujihusisha na shughuli za maendeleo.”

Mkutano huo ni moja ya maandalizi ya Mkutano wa  69 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UN) unaotarajiwa kufunguliwa tarehe 24/9/2014 mjini humo.