Mama Kanumba Alia Ukumbini…!

Mama yake na marehemu Steven Kanumba akilia baada ya kuitwa akapokee tuzo ya mwanaye kwenye tuzo za Filamu 2015.

Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa wa mwanaye kwenye tasnia ya filamu aliyoitwaa kwenye tuzo za Filamu 2015. Tuzo hiyo ilimgusa na kujikuta akiangua kilio ukumbini juzi.

MAMA wa aliyekuwa staa wa filamu nchini Tanzania Steven Kanumba (The Great) juzi jijini Dar es Salaam alijikuta akiangua kilio hadharani kwenye hafla ya utoaji Tuzo za Filamu Tanzania kwa mwaka 2015 (Tuzo za TAFA 2015).

Tukio hilo lilitokea mara baada ya kutangazwa kwa marehemu Steven Kanumba kutwaa tuzo ya msanii aliyechangia kiasi kikubwa kukua kwa tasnia ya filamu nchini kwa mwka 2015. Mama wa staa hiyo alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio cha kuguswa na kitendo cha mwanaye kuendelea kutambuliwa katika tasnia hiyo licha ya kutokuwepo.

Baada ya tukio hilo wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu walionekana kumzingira huku wakimpa hongera na wengine kumtuliza na kitendo cha kububujikwa na machozi. Staa wa filamu Kanumba alifariki dunia usiku wa Aprili 7, 2012 akiwa na umri wa miaka 28, ambapo msiba wake ulivuta hisia za Watanzania wengi hasa wapenzi wa tasnia ya filamu. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 20,000 walihudhuria mazishi ya staa huyo wa filamu nchini Tanzania.

Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa wa mwanaye kwenye tasnia ya filamu aliyoitwaa kwenye tuzo za Filamu 2015. Tuzo hiyo ilimgusa na kujikuta akiangua kilio ukumbini juzi.

Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa wa mwanaye kwenye tasnia ya filamu aliyoitwaa kwenye tuzo za Filamu 2015. Tuzo hiyo ilimgusa na kujikuta akiangua kilio ukumbini juzi.

Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akiwa imegeuka kutazama tukio la mama Kanumba kububujikwa na machozi mara baada ya mama wa staa huyo kuitwa akapokee tuzo ya mwanaye kwenye tuzo za Filamu 2015.

Mama yake na Steven Kanumba akiwarijiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 juzi.

Mama yake na Steven Kanumba akiwarijiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 juzi. Picha zote na dev.kisakuzi.com.