Mama Bilal ahudhuria maadhimisho ya miaka 20 ya COWPZ

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) Balozi Amina Salum Ally, kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kusimamia Jumuiya hiyo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar Novemba 26.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, (wa pili kushoto) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Awena Seif (kushoto) na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, wakisikiliza maelezo kutoka kwa mjasiliamali , Biubwa Said aliyekuwa akiwaelezea jinsi ya kuandaa Clips za Viazi, Mihogo na Tambi za Unga wa Dengu, wakati wa fanyabiashara wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar Novemba 26.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wakazi waliohudhuria maadhimisho ya sherehe hizo za miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipokea maandamano ya Wanawake na Vijana, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ) zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bustani ya Victoria mjini Zanzibar jana Novemba 26.


Mama Bilal akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Jumuiya ya Kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake Zanzibar (COWPZ)