Mama Asha Bilal ufungua semina ya ‘Arts Association’

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Tuzo na zawadi, Mc Marry Mwanyato, aliyefanya vizuri kwa mwaka 2011-2012, wakati wa ufunguzi wa Semina elekezi ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha ‘Sherehe Arts Association’ (SAA), kujadili changamoto mbalimbali zinazolikabili soko la Biashara, kukuza ubunifu wa sanaa kwa wateja, masoko na elimu ya mitandao ya Kijamii. Semina hiyo iliyofunguliwa na Mama Asha Bilal, ilifanyika Septemba 10, 2012. Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha ‘Sherehe Arts Association’ (SAA) baada ya ufunguzi wa Semina elekezi ya siku moja iliyoandaliwa na chama hicho kujadili changamoto mbalimbali zinazolikabili soko la Biashara, kukuza ubunifu wa sanaa kwa wateja, masoko na elimu ya mitandao ya Kijamii. Semina hiyo iliyofunguliwa na Mama Asha Bilal, ilifanyika Septemba 10, 2012. Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR