Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimpongeza kwa kumpa taji la maua mtoto wa dada yake, Musiba Mshimba, aliyehitimu katika Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki baada ya kutunukiwa cheti cha kuhitimu mafunzo ya Doctor Of Medicine wakati wa mahafali ya 9 ya chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana.
Baadhi ya wahitimu wakila kiapo wakati wa mahafali hayo walipokuwa wakitunukiwa vyeti.
Mama Asha Bilal, Ndugu Jamaa na Marafiki wakimpongeza Musiba Mshimba katika sherehe ya mahafali yake.