
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam, Desemba 12, baada ya kumaliza shughuli ya hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Msaafu kutoka kwa, Sheikh Ahmed Mohamed Lbadry, baada ya kumaliza hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la dar es Salaam na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Desemba 12.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa halfa ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tanzania Tawi la Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika Desemba 11, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee jijini.