Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria cha Zanzibar Tanzania, Grace Kissassi, wakati alipokutana naye baada ya kufungua rasmi mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika, kuhusu elimu ya mafunzo ya masafa uliofunguliwa rasmi leo Julai 13, 2011 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika, uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini wakifuatilia hotuba ya Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Zambia nchini, Mavis Lengalenga, baada ya kuzindua rasmi mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la Wakuu wa vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu, uliofunguliwa leo Julai 13 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa mkuu wa tatu wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu kuhusu Elimu ya mafunzo ya Masafa uliofunguliwa lei Julai 13 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Picha na Muhidin Sufiani-OMR