Makamu wa Rais Dk Bilal, Magufuli, RC Dar na Kova Wanusurika Kifo Ajali ya Helkopita

Helkopita hiyo ya Jeshi ikiwa imeanguka chini muda mfupi baada ya kuruka.

Helkopita hiyo ya Jeshi ikiwa imeanguka chini muda mfupi baada ya kuruka.

Gari la zimamoto likiimwagia maji mara baada ya kuanguka kuzuia madhara zaidi helkopita hiyo.

Gari la zimamoto likiimwagia maji mara baada ya kuanguka kuzuia madhara zaidi helkopita hiyo.

Helkopita hiyo ya Jeshi ikiwa imeanguka chini muda mfupi baada ya kuruka.

Helkopita hiyo ya Jeshi ikiwa imeanguka chini muda mfupi baada ya kuruka.

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dk.John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiki pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova wamenusurika kufa baada ya helkopta ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliyokuwa wakiitumia kupata hitlafu na kuanguka eneo la Jeshi leo.

Tukio hilo limetokea leo jijini Dar es Salaam baada ya helkopita hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kuanza kuruka ikielekea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na ilikuwa pia impeleke Makamu wa Rais mikoa ya jirani ukiwemo Morogoro kuangalia athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa Dar es Salaam na mikoa jirani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilisema hata hivyo helkopita hiyo baada ya kuruka haikwenda mbali kabla ya kutokea tatizo hilo na kuanguka eneo la Jeshi jijini Dar es Salaam jirani na Uwanja wa Zamani wa Ndege (Teminal One) na ndani ya Jeshi la Wananchi Tanzania. Ndege hiyo ambayo pia ilikuwa imewabeba wanausalama na wanahabari walioambatana na Makamu wa Rais iliwahiwa na gari la kikosi cha zimamoto na kumwagiwa maji baada ya kuanguka ili kuzuia madhara zaidi kutokea baada ya ajali hiyo.

Taarifa zinasema hata hivyo, msafara wa Makamu wa Rais Dk. Bilal uliendelea na kazi ya kukagua maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa mfululizo zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kwa kutumia magari baada ya zoezi la helkopita kushindikana kwa ajali.

Kwa mujibu wa chazo chetu, hakuna madhara makubwa kwa viongozi na watu wengine waliokuwa katika helkopita hiyo ilipopata ajali na ndiyo maana ziara iliendelea kwa kutumia magari badala ya helkopita kama ilivyokuwa awali. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mtandao huu.