Makamu wa Rais, Dk. Bilal Azindua Jengo la DHL Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkurugenzi Mkuu wa DHL, Blaise D’sauza, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuwashiria uzinduzi wa jengo jipya la Kampuni ya Usafirishaji wa Mizigo ndani na nje ya nchi (DHL), wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika Desemba 07, 2012, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa DHL, Blaise D’sauza, wakati alipokuwa akitembelea katika jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, (DHL) baada ya kuzindua rasmi jengo hilo lililopo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Desemba, 07, 2012. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa DHL, Blaise D’sauza, mara baada ya uzinduzi wa jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, (DHL) lililopo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Desemba, 07, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki. Picha na OMR