Makamu wa Rais Aongoza Kampeni ya Upandaji Miti Dar

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipanda mti kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam 'Mti wangu'

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipanda mti kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam ‘Mti wangu’

 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipanda mti kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam 'Mti wangu'

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipanda mti kuashiria uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam ‘Mti wangu’

 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam 'Mti wangu'

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam ‘Mti wangu’

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN leo tarehe 1-Oct-2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.

 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na wanafunzi kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam 'Mti wangu'

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na wanafunzi kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam ‘Mti wangu’

 

Amesema kuwa jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti iliyopandwa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya viongozi katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam 'Mti wangu'

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya viongozi katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti Dar es Salaam ‘Mti wangu’

 

Amesema anafaraja na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.

Baada ya kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.