Makampuni ya Mafuta Kusaidia Tanzania Kunufaika na Sekta ya Gesi na Mafuta

Mkuu wa Kitengo cha Mikataba na Ununuzi wa BG East Africa David Johnson akijibu swali la mmoja wa wageni waliohudhuria hafla hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mikataba na Ununuzi wa BG East Africa David Johnson akijibu swali la mmoja wa wageni waliohudhuria hafla hiyo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa Kampuni ya Pietro Firentini, Abdul;samad Abdulrahim akiuliza swali katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Programmu wa Kampuni ya Achilles, Christopher House akijibu maswali ya baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.



MAKAMPUNI MAKUBWA YA MAFUTA KUSAIDIA TANZANIA KUNUFAIKA NA SEKTA YA GESI NA MAFUTA


Dar es Salaam – Thursday January 28, 2016; Wakati fursa za biashara za mabilioni  ya shilingi zikiendelea kuibuka katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini, Wafanyabiashara na makampuni yenye dhamira ya kutoa huduma za mafuta na gesi nchini wamepatiwa fursa mpya kujitangaza duniani kote hususan kwa makampuni makubwa ya mafuta ambayo yanahitaji wadau wa kushirikiana nao katika biashara hiyo hapa nchini.


Huku ikikadiriwa kuwa na takriban futi za ujazo Trilioni 55 za gesi asilia, Tanzania inaonekana kwenye jicho la biashara hiyo kimataifa kama mdau muhimu anayechipukia na eneo lenye fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi.


Katika hatua ya aina yake, ambayo ni sehemu ya mpango mkakati wa muda mreffu, makampuni maakubwa ya mafuta BG Tanzania, Statoil Tanzania AS kwa kushirikiana na lile la mtandao la Achilles wamezindua mfumo mpya wa kimtandao  kuhusu Tanzania utakaotumika kama njia rahisi ya kutambua na kuchagua makampuni ya ndani yanayofanya biashara ya mafuta na gesi kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali za kibiashara kote ulimwenguni.


Makampuni hayo yamekubaliana kuwa na utaratibu mmoja kwenye utambuzi wa wa makampuni yanayofanya biashara hiyo hapa nchini. Utaratibu huo unazingatia viwango vinavyokubalika ambavyo watoa huduma wote wanapaswa kuwa navyo ili waweze kuwepo kwenye mfumo huo wa utambuzi na kunufaika na fursa zinazopatikana. Katika hatua ya awali, makampuni ya mafuta na gesi yatapaswa kuwasilisha taarifa muhimu zinazohitajika kuhusu hali yao ya kibiashara na mambo ya kimsingi kama afya, usalama, mazingira na huduma za jamii. Taarifa hizi zitaingizwa moja kwa moja kwenye mtandao.


Kwa taarifa hizo, washirika wataweza kutambua wabia muafaka na kuweza kushirikiana katika kujenga uwezo hususan katika kuala la viwango na kushughulikia suala la mahitaji na taratibu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo. Pia kwa kuwa na usajili huu na mfumo wa pamoja watoa wasambazaji wanaweza kuwasiliana na kufanya kazi na wanunuzi waliopo kwenye.


Gareth Palmer, Mkurugenzi wa Achilles Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika, ambao wanafanya kazi kwa niaba ya takriban mashirika 200 ya ununuzi wa mafuta na gesi kote duniani amesema  “kwa kuweka na kutumia utaratibu huu wa kimtandao, BG na Statoil wanarahisisha sana uwezo wa makampuni ya hapa nchini kujitangaza na kuweza kupata wabia mbalimbali na kupanua wigo wa fursa za kibiashara”


Naye John Ulanga, Afisa muandamizi wa BG Tanzania amesema  “Kuwasaidia na kuwaunga mkono wafanyabiashara katika sekta hii hapa nchini in maana kubwa sana kibiashara. Kwa msingi huu tunafurahi kuwekeza katika mfumo huu muhimu hapa nchini na nje pia. Kwa kutumia mfumo huu tunatumaini kuwa tutaweza kuzitambua, kuzisaidia na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania kwa wadau wa kote duniani”


Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano wa Statoil Tanzania AS  Genevieve Kassanga amesema  kwa wamefurahishwa sana na kukamilika kwa mfumo huu muhimu ambao utawawezesha wauzaji na wanunuzi kote Tanzania kuweza kutambulika na kufunguliwa kwa fursa za kufanya biashara kwa ufanisi zaidi. “Tunaamini kuwa ushirikiano huu utachochea ukuaji wa makampuni ya ndani na kuchangia kwa kasi zaidi katika ukuaji wa uchumi wa nchi.


Godfrey Simbeye Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF amesema mtandao huo ni suluhisho kubwa kwa wawekezaji wazawa katika sekta ya mafuta na gesi kwani utawawezesha kufahamika na kueleweka kote duniani. Ametoa rai kwa wadau kuhakikisha kuwa gharama za kujiunga na mtandao huo ni ndogo ili kuyawezesha makampuni ya kiz