Mwenyekiti Mwenza ukawa Emmanuel Makaidi afariki leo katika hospitali ya Nyagao, lindi kwa shinikizo la damu mkwewe bi Modesta Makaidi athibitisha.
Kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo mtandao huu umezipata, Makaidi amefariki dunia akipata matibabu katika hospitali ya Nyagao iliyopo Mkoani Lindi. Kufariki kwa Makaidi aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha NLD itakuwa ni pigo kwa vyama washirika vinavyounda umoja wa ukawa ambao walikuwa wakishirikiana kwa kuungana mkono katika uchanguzi huu kwa vyama vya Chadema, CUF,NCCR-Mageuzi pamoja na NLD yenyewe. Taarifa zaidi ni hapo baadae